Ni mfumo wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu uliowezeshwa kwa ushirikiano wa Airtel na Veta. Mwanafunzi atasoma mafunzo ya nadharia kwa kutumia VSOMO App kwenye simu yake ya mkononi na kujiunga na mafunzo ya vitendo kwenye kituo cha VETA kilicho karibu naye nchi nzima.

Jinsi ya kujiunga na VSOMO

Kwa kutumia smartphone yako ya Android, pakua App ya Vsomo kupitia Google playstore na ujisajili BURE, kisha chagua kozi yoyote ya ufundi unayohitaji.

Muda wa masomo

Mafunzo ya nadhari yanapatikana kupitia simu yako ya mkononi kwa muda wowote. Mafunzo ya vitendo yanapatikana katika kituo cha veta kilichopo karibu nawe nchi nzima . Mafunzo hayo hutolewa kwa muda wa wiki mbili, kwa siku ni masaa sita ya masomo.

Vigezo na masharti

 • Gharama ya kila kozi ni Tsh 120,000/= ambayo ni punguzo la 60%.
 • Wahitimu kutunukiwa cheti na mamlaka ya ufundi stadi nchini VETA
 • Kulipia kupitia Airtel Money piga *150*60#
 • Kwa sasa huduma hii ni kwa wateja wa Airtel tu.

Kozi za VSOMO

 • Misingi Ya Ufundi Wa Pikipiki
 • Kuweka Umeme
 • Ufundi Wa Simu za mikononi
 • Kuchomelea Na Kuunda Vyuma
 • Urembo
 • Kutengeneza Maumbo Ya Alumini Na Upvc
 • Umeme Wa Magari
 • Ufundi Bomba Wa Majumbani
 • Umeme Wa Viwandani
 • Matengenezo Ya Kompyuta
 • Huduma Ya Chakula Na Mbinu Za Kuhudumia Wateja
 • Kuoka Na Kupamba Keki

Kwa Maelezo Zaidi:

Tafadhali piga namba zifuatazo kupata maelezo zaidi ya namna ya kujiunga na kozi zinazotolewa kwa njia ya VSomo

+255 699 859 572
+255 699 859 573