News & Events

Events


Sherehe za Uzinduzi wa Chuo Cha TEHAMA - VETA Kipawa


Mkuu wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa, Mhandisi Lucius R. Luteganya akifurahi kuwakaribisha Wageni Maalum katika Sherehe za Uzinduzi.

Waziri wa Elimu, Dr. Shukuru Kawambwa, (wa pili kushoto) akiwasili katika Sherehe za Uzinduzi na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya VETA - Tanzania, Prof. Idris Msholo (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa VETA - Tanzania, Eng. Zebedia Moshi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, Mrs. Ndunguru.


Waziri wa Elimu, Dr. Shukuru Kawambwa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya VETA - Tanzania, Prof. Idris Msholo wakati wa sherehe za Uzinduzi.

Burudani ya Ngoma na sarakasi ikiendelea wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa.


Waziri wa Elimu, Dr. Shukuru Kawambwa akifurahia jambo, pamoja na Mkurugenzi wa VETA - Tanzania, Eng. Zebedia Moshi wakati wakisubiri kumpokea Mgeni Rasmi wa Sherehe za Uzinduzi.

Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Sherehe za Uzinduzi wa Taasisi ya TEHAMA, VETA -Kipawa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za Uzinduzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa VETA - Kanda ya Dar es Salaam, Mrs Ndunguru.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa, Eng. Lucius R. Luteganya, wakati akiwasili sherehe za Uzinduzi.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA - Tanzania, Eng. Zebedia Moshi akitoa Risala inayohusu Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Taasisi ya VETA - Kipawa, kwa Mgeni Rasmi, Rais Jakaya M. Kikwete (hayupo pichani)


Baadhi ya wageni waalikwa na wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea katika sherehe za uzinduzi wa Taasisi ya TEHAMA - VETA Kipawa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick akiwasilisha salamu za wananchi wa Dar es Salaam kwa Mgeni Rasmi, Mh. Dr. Jakaya M. Kikwete.


Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Hon. Chung IL, akisoma Risala inayohusu mradi wa Ujenzi wa Taasisi ya VETA - Kipawa kwa kushiriana na serikali ya Korea Kusini.

Waziri wa Elimu, Dr. Shukuru Kawambwa akimkaribisha Mgeni Rasmi, Dr. Jakaya M. Kikwete katika Sherehe za Ufunguzi wa Taasisi ya TEHAMA VETA Kipawa.
Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akitoa hotuba katika Sherehe za uzinduzi wa Chuo cha TEHAMA VETA - Kipawa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akibonyeza kitufe, ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, akikata utepe, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya VETA - Tanzania, akikabidhi zawadi ya "Power Backup" iliyotengenezwa na Taasisi ya TEHAMA, VETA Kipawa kwa Mgeni Rasmi, Rais ya Tanzania Mh. Jakaya M. Kikwete


Mwalimu wa Umeme, Mrs Eunice Urio, akitoa maelezo kwa Rais Kikwete kuhusu moja ya vifaa vya kufundishia fani ya umeme katika maabara ya Umeme.

Mwalimu wa Ufundi wa Elektroniki, Mr. Ricky Sambo, akimfafanulia jambo Mhe. Rais wakati alipotembelea maabara ya kufundishia fani ya Elektroniki.


Rais Kikwete akitazama namna mifumo ya ki-elektronic inayofanya kazi katika computer, wakati Mwalimu wa fani hiyo, Mr. Ricky Sambo akionesha jinsi mifumo hiyo inavyofanya kazi.

Mwalimu wa Ufundi wa Elektroniki, Mr. Ricky Sambo, akimfafanulia jambo Mhe. Rais wakati alipotembelea maabara ya kufundishia fani ya Elektroniki.


Rais Kikwete akimsikiliza Mwalimu wa fani ya Umeme, Mr. Adrian Aloyce akifafanua namna mtambo wa umeme wa viwandani unavyofanya kazi.

Msimamizi wa mafunzo kwa njia ya Mtandao (E-learning) na mwalimu wa Sayansi ya Uhandisi, Mr. Martin Choma, akitoa maelezo kwa Rais Jakaya Kikwete ya namna mafunzo kwa njia ya mtandao yanavyoweza kutolewa katika Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa.


Mwalimu wa fani ya Multimedia, Mr. Kasuma H. Nchimbi akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi, Rais Jakaya M. Kikwete kuhusu mafunzo yanayofundishwa katika fani hiyo.

Rais Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa, mara baada ya kuzindua Chuo hicho.


Viongozi Wakuu wa VETA wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya M. Kikwete, mara baada ya Uzinduzi wa Taasisi ya TEHAMA VETA Kipawa.

Baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo vya VETA Kipawa IICT na Dar es Salaam RVTSC wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Rais Kikwete.


Rais Kikwete akitazama burudani iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya sherehe za uzinduzi.

Rais Kikwete akiagana na baadhi ya viongozi, kabla ya kuondoka katika sherehe za uzinduzi wa Chuo cha TEHAMA VETA Kipawa.