News & Events

News


VSomo - Mafunzo kwa njia ya mtandao!

 1. VSomo ni nini?
 2. VSomo ni mfumo wa kwanza wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya mtandao Tanzania. Umeanzishwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) pamoja na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA.
  VSomo yaani VETA Somo ni program tumishi (application) mpya inayokuwezesha kupata mafunzo yanayotolewa na Vyuo vya VETA kupitia simu yako ya mkononi (Smart Phone).

 3. VSomo inapatikana wapi?
 4. Vsomo inapatikana kupitia simu yako ya mkononi ya kisasa (Smart Phone), katika moja ya programu tumishi (Applications) ambazo hupatikana katika "Play Store"?
  Katika simu yako ya kisasa, nenda kwenye "Play Store", utatafuta "VSomo", utaipakua (download), na kufuata maelekezo yatakayotolewa.

 5. Jinsi gani Mafunzo hutolewa kwa VSomo?
 6. Unapopakua program tumishi ya VSomo, utatakiwa kujisajili. Ukishakamilisha taratibu zote, na kuchagua kozi unayotaka kusoma, utaanza kusoma. Pia utatakiwa kujibu maswali yatakayotolewa katika kuendelea kujifunza. Baada ya kumaliza kusoma, utatakiwa kuchagua chuo chochote cha VETA kilicho karibu nawe ili kuja kupata mafunzo ya Vitendo na kufanya mtihani. Ukishafaulu hapo, utapewa cheti cha kuhitimu.

 7. Ninatakiwa kuwa na nini ili kusoma kwa njia ya VSomo?
 8. Unatakiwa kuwa na simu ya kisasa (Smart Phone) na namba ya mtandao wa Airtel.

 9. Nitapataje Maelezo zaidi kuhusu VSomo?
 10. Tafadhali piga namba zifuatazo kupata maelezo zaidi ya namna ya kujiunga na kozi zinazotolewa kwa njia ya VSomo.
  +255 22 2843360
  +255 754 949250