Kozi Maalum ya Ufundi wa Simu (Mobile Phone)

Mkuu wa Chuo cha TEHAMA cha VETA Kipawa (VETA Kipawa ICT Centre) anatangaza nafazi za mafunzo ya ufundi wa simu kwa wanafunzi 400. Mafunzo haya ni BURE na yatatolewa kwa muda wa wiki sita (6).

Mafunzo yatatolewa katika hatua tatu ambazo ni:-
  1. Hatua ya Awali (BASIC)
  2. Hatua ya Kati (INTERMEDIATE)
  3. Hatua ya Juu (ADVANCED)

Mhitimu wa kozi hii atakuwa na ujuzi wa yafuatayo:-
  1. Misingi ya utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki
  2. Kutambua na kutatua matatizo ya simu za mikononi (HARDWARE & SOFTWARE)
  3. Sheria, taratibu na kanuni za Mawasiliano zinazoongoza tasnia nzima ya ufundi wa Simu
  4. Ujasiriamali
Mwanafunzi atakapofaulu atatunukiwa CHETI kutoka VETA kitakachomuwezesha kupata LESENI kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Leseni hii itamuwezesha kufanya kazi za ufundi wa simu (Mobile Phones).

Mafunzo yatafanyika katika chuo cha TEHAMA VETA Kipawa kilichopo Mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala, Kata ya Kipawa. Chuo kiko mkabala na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere, karibu na reli ya kati. Kinapakana na Zahanati ya Kipawa, na shule ya Sekondari Ilala.

Mafunzo haya yanatolewa kwa UFADHILI wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) chini ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Fomu za maombi ya ufadhili itajazwa kwa njia ya mtandao (online) kupitia kiunganishi Ufundi Simu au Tembelea tovuti ya Chuo, www.vetakipawa.ac.tz. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15/07/2020.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba: 0714 720 381.

IMETOLEWA NA MKUU WA CHUO - VETA KIPAWA ICT CENTRE.