Short Course Student

Nashukuru Sana kwa Waziri Mkuu kutupa nafasi hii vijana ili kujikwamua kimaisha napia kupata ujuzi na kuongeza ufanisi katika kazi. Na pia natoa shukrani kwa chuo cha Veta Kipawa ICTC, katika kutusimamia vema vijana katika ujuzi na ufanisi. Shukrani zangu kwa uwongozi wote wa chuo na walimu kwa ujumla niseme Asante Mungu awabariki Sana. Ujuzi niliopata umenisaidia kujiajili mwenyewe na kupata kipato kinachoweza kunisaidia katika maendeleo yangu na jamii kwa ujumla. Nawashauri vijana wenzangu msikate tamaa maana nafasi bado zipo ili kuweza kutimiza malengo yetu.

X