School Rules

1. MAHUDHURIO
Unatakiwa kufika chuoni kabla ya saa 1:30 asubuhi. Hii inamaana ifikapo saa 1:30 wanafunzi wote muwe mmeshafika chuoni. Hatua kali ya kinidhamu itachukuliwa kwa wachelewaji.

Hutakiwi kutoka nje ya chuo kwenda nyumbani, hospitali au sehemu nyingine yoyote ile, bila ya kuruhusiwa na (Mkuu wa sehemu au mwalimu wa darasa).
(c) Upatapo matatizo ya msiba, kuuguliwa au kuugua mwenyewe nilazima habari/taarifa zifike chuoni, bila ya kufanya hivyo ni kosa.
(d) Mahudhurio chini ya 85%, utakosa sifa ya kuhitimu na hutaruhusiwa kufanya mtihani wa Taifa.

2. MAVAZI
Sare ya chuo ni suruali ya Blue na shati Jeupe mikono mirefu/T-shirt (Flana). Sare hiyo uivae wakati wote, uwapo chuoni na wakati wa safari ya kuja chuoni na kurudi nyumbani. Wakati wote shati liwe limechomekewa na liwe na nembo ya VETA. Flana uivae siku ya Jumatano na Ijumaa tu.

Ovakoti ulivae wakati wa vipindi vya kazi za mikono tu.

Viatu vyenye visigino virefu, kandambili au viatu vya wazi (Sandals) huruhusiwi kuvivaa uwapo chuoni.

3. USAFI WA MWILI
Huruhusiwi kuvaa hereni, pete, bangili, mkufu na mapambo ya aina yoyote ile kwa kipindi chote cha mafunzo.

Nywele Kwa Wavulana:-
Uzikate ziwe fupi sana, Kipara, Panki huruhusiwi kabisa.
Huruhusiwi kufuga ndevu (Sharubu, sharafa, ndevu kidevuni na kionja mchuzi).
(c) Nywele Kwa Wasichana
Uzikate zisiwe fupi sana, Kipara, Panki huruhusiwi kabisa au
Zisuke kwa mistari ya kurudi nyuma.

Huruhusiwi kufuga wala kupaka rangi kucha.

4. USAFI WA MAZINGIRA
Unatakiwa kuhakikisha maeneo yote yanayokuzunguka ni masafi, kwa kuokota uchafu wowote utakaouona na kuweka sehemu husika za kutupa taka.

Ni marufuku kushika au kukanyaga kuta za jengo; uwapo karakana au darasani ama nje.

Ni marufuku kuingia darasani au karakana na aina yoyote ya kimiminika, chakula, bazoka nk.

Huruhusiwi kupita kwenye eneo la katikati (Corridor) ya Ofisi za Utawala pindi uendapo kantini isipokuwa unapokuwa nashida ya kiofisi.

Huruhusiwi kukatisha katika sehemu za bustani za mauaau sehemu zilizopandwa nyasi, unatakiwa kutumia njia husika (Pavement).

5. WIZI WA MALI ZA CHUO AU MALI YA MTU YEYOTE YULE:
(a) Vitendo vyovyote vya wizi haviruhusiwi. Pindi ikibainika mwanafunzi umeiba mali ya chuo au ya mwanafunzi mwenzako, hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa chuoni.
NB: Kifaa au mali yeyote isiyo ya chuo unatakiwa uiandikishe na ikaguliwe getini kwa walinzi kabla ya kuingia darasani na baada ya kutoka darasani.

(b) Usafi wa maeneo yote ya chuo ni wajibu wa kila mwanafunzi hivyo unawajibika kila wakati kutunza bustani, maeneo yote ya ndani na nje ya chuo kuwa safi daima.

X