MRADI WA KUKUZA AJIRA NA UJUZI-TANZANIA
(EMPLOYMENT AND SKILLS FOR DEVELOPMENT-TANZANIA)
TAARIFA KWA UMMA
FURSA YA MAFUNZO YA UKUZAJI UJUZI KATIKA FANI YA MEKATRONIKI
1. UTANGULIZI
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu –
Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kutekeleza
mradi wa Kukuza Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo ya Afrika (E4D). Mradi unalenga kuwezesha utoaji
wa mafunzo ya ufundi stadi katika fani ya Mekatroniki (mechatronics), kwa vijana 32 wenye umri
kati ya miaka 15 hadi 35.
Mradi wa E4D unafadhiliwa na Wizara ya Shirikisho la Ujerumani ya Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo (BMZ), Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo wa Norway (Norad), Umoja wa Ulaya
(EU) na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Korea ya Kusini (KOICA).
Mafunzo yatatolewa katika Chuo cha TEHAMA cha VETA Kipawa kilichopo eneo la Karakata, Dar
es salaam, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA).
2. VIGEZO VYA KUJIUNGA NA FANI
Mwombaji wa mafunzo hayo anatakiwa kukidhi vigezo vifuatavyo:
(i) Uwe raia wa Tanzania.
(ii) Uwe na umri wa kati ya miaka 15 hadi 35 (Idhini ya maandishi ya wazazi/walezi
inahitajika wa watu kati ya umri wa miaka 15 hadi 18 wakati wa mafunzo ya vitendo
viwandani.)
(iii) Awe na ujuzi au uzoefu wa walau mwaka mmoja katika mojawapo ya fani za TEHAMA,
Umeme, Elektroniki au Mekaniko.
(iv) Awe tayari kuhudhuria mafunzo katika Chuo cha TEHAMA cha VETA, KIPAWA katika
muda wote.
Kwa taarifa zaidi, bofya: https://bit.ly/46bfHtX
(1) Comment